Cape Verde yaweka rekodi mechi ya Kwanza Kombe la Dunia ikitoshana nguvu na Hispania

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th June 2026


Cape Verde yaweka rekodi mechi ya Kwanza Kombe la Dunia ikitoshana nguvu na Hispania

Timu ya taifa ya Cape Verde imeandika historia katika Kombe la Dunia 2026 baada ya kuizuia Hispania kwa sare ya bila kufungana (0-0) kwenye mechi ya ufunguzi ya Kundi H. Matokeo hayo yameifanya Cape Verde kuokota alama yake ya kwanza kabisa katika historia ya mashindano hayo huku ikiweka rekodi katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia.

Cape Verde, ambayo inashiriki Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika historia yake, ilionyesha nidhamu kubwa ya kiulinzi dhidi ya moja ya timu zinazopewa nafasi ya kutwaa ubingwa. Licha ya Hispania kumiliki mpira kwa muda mrefu na kutengeneza nafasi kadhaa za kufunga, safu ya ulinzi ya Cape Verde pamoja na kipa mkongwe Vozinha waliweza kuhimili mashambulizi yote na kuhakikisha timu yao inaondoka na pointi muhimu.

Kipa Vozinha mwenye umri wa miaka 40 alikuwa nyota mchezo huo. Ameandika historia pia kwa kuwa mmoja wa wachezaji wenye umri mkubwa zaidi kucheza mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia. Uchezaji wake bora uliwavutia mashabiki wengi akipata umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii.

Kocha wa Cape Verde, Pedro "Bubista" Brito, alisema kabla ya mchezo kwamba timu yake haikuja Kombe la Dunia kwa ajili ya kushiriki tu bali kushindana. Kauli hiyo ilidhihirika uwanjani baada ya wachezaji wake kuonyesha moyo wa kupambana dhidi ya mabingwa wa Ulaya.

Matokeo hayo yanaifanya Cape Verde kupata alama moja muhimu katika Kundi H, ambalo pia lina timu za Uruguay na Saudi Arabia. Sare hiyo imeipa Cape Verde matumaini ya kuendelea kupambana kwa nafasi ya kufuzu hatua inayofuata katika mashindano hayo.

Kwa upande wa Hispania, sare hiyo imeonekana kama matokeo ya kushtua kwa mashabiki wake kwani ni mechi ambayo walitarajia kuibuka na ushhindi mnono.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.