Coastal Union yaichapa KMC mabao 3-1 KMC Complex

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th June 2026


Coastal Union yaichapa KMC mabao 3-1 KMC Complex

Coastal Union (Wagosi wa Kaya) wameondoka na pointi tatu muhimu baada ya kuifunga KMC FC mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye dimba la KMC Complex.

Mchezo huo ambao KMC walikuwa wakitimiza ratiba baada ya kuthibitika kushuka daraja, ulitawaliwa zaidi na Coastal Union waliokuwa na ari na umakini wa kupata matokeo muhimu katika vita ya kujinusuru na presha ya kushuka daraja.

Coastal Union walianza kwa kasi na kupata bao la mapema dakika ya 3 kupitia kwa Robert Pius, kabla ya kuongeza la pili dakika ya 7 kupitia kwa Greyson Gwalala, hali iliyoziweka KMC kwenye wakati mgumu mapema kabisa.

KMC walijibu dakika ya 30 kupitia kwa Mudathir Nassor, ambaye aliipa timu yake bao la kufutia machozi kupitia mkwaju wa penati baada ya juhudi za kurejea mchezoni kuanza kuonekana.

Hata hivyo, Coastal Union walidhibiti mchezo kwa umakini mkubwa hadi kipindi cha pili, huku KMC wakishindwa kutumia nafasi walizopata kusawazisha.

Kipindi cha pili kilishuhudia Coastal Union wakiendelea kushambulia kwa tahadhari, kabla ya kupata bao la tatu dakika ya 88 kupitia kwa Thomas Ulimwengu, likihitimisha ushindi huo wa ugenini.

Kwa matokeo hayo, Coastal Union wamefikisha alama 32, wakijiweka katika nafasi salama zaidi kwenye msimamo wa ligi, wakati KMC wakiendelea kusalia chini ya msimamo baada ya kushuka daraja.

Ushindi huo unazidi kuongeza matumaini kwa Coastal Union kuelekea mechi zao zilizobaki msimu huu, huku wakiendelea kupambana kuepuka hatari ya kushuka daraja.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.