Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mechi mbili za kuhitimisha raundi ya 26 zitapigwa.
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc watakuwa uwanja wa nyumbani KMC Complex kuikabili Pamba Jiji katika mchezo unaotarajiwa kuwa na upinzani mkali.
Simba inahitaji ushindi ili kusalia kwenye mbio za ubingwa huku Pamba Jiji nao wakihitaji alama tatu ili kujiimarisha katika mapambano yao ya kuwania nafasi nne za juu.
Mara ya mwisho timu hizo zilipokutana uwanja wa CCM Kirumba zilitoshana nguvu kwa matokeo ya sare ya bao 1-1.
Mchezo mwingine unaotarajiwa kupigwa leo ni kati ya Pamba Jiji dhidi ya Dodoma Jiji dimba la Sokoine mkoani Mbeya.
Tanzania Prisons wako kwenye hatari ya kuungana na KMC kushuka daraja msimu huu hivyo ni mchezo ambao wanahitaji ushindi ili kuweka hai matumaini yao ya kusalia ligi kuu.




