Kombe la Dunia 2026; Canada yapata pointi ya kwanza, Marekani yatoa onyo

Joel JJ By Joel JJ β€’ 13th June 2026


Kombe la Dunia 2026; Canada yapata pointi ya kwanza, Marekani yatoa onyo

Kombe la Dunia 2026 limeanza kwa shamrashamra kubwa huku mataifa mbalimbali yakianza safari ya kusaka ubingwa wa dunia. Mechi mbili zimeshuhudiwa usiku wa Ijumaa na Alfajiri ya Jumamosi katika makundi B na D.

Timu mwenyeji Canada ilianza kampeni yake kwa sare ya mabao 1-1 dhidi ya Bosnia na Herzegovina katika mechi iliyopigwa Toronto.

Bosnia walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia Jovo Lukic kabla ya mshambuliaji Cyle Larin kuisawazishia Canada muda mfupi baada ya kuingia uwanjani kama mchezaji wa akiba.

Matokeo hayo yameiwezesha Canada kupata pointi yake ya kwanza kabisa katika historia ya ushiriki wao wa Kombe la Dunia la wanaume.

Kwa sasa, mechi nyingine ya kundi B kati ya Qatar na Switzerland itachezwa leo tarehe 13 Juni 2026.Β 

Msimamo wa Awali Kundi B

  • Canada – Pointi 1

  • Bosnia na Herzegovina – Pointi 1

  • Qatar – 

  • Switzerland – 

Kundi D: Marekani Yatoa Onyo kwa Wapinzani

Kundi D limeanza kwa kishindo baada ya Marekani kuifunga Paraguay mabao 4-1 katika mchezo wa ufunguzi wa kundi hilo. Folarin Balogun alikuwa nyota wa mchezo huo kwa kufunga mabao mawili, huku Gio Reyna akiongeza bao jingine na Paraguay kujikuta ikizidiwa katika maeneo mengi ya uwanja. Ushindi huo umeifanya Marekani kuongoza kundi mapema na kuonyesha dhamira ya kufanya vizuri mbele ya mashabiki wake wa nyumbani.

Msimamo wa Awali Kundi D

  • Marekani – Pointi 3

  • Paraguay – Pointi 0

  • Australia – 

  • Uturuki – 


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.