Taharuki kambi ya Ureno: ripoti za kuonekana kwa mamba zazua hofu

Joel JJ By Joel JJ β€’ 12th June 2026


Taharuki kambi ya Ureno: ripoti za kuonekana kwa mamba zazua hofu

Hali ya taharuki imeripotiwa kutanda katika kambi ya mazoezi ya timu ya taifa ya Ureno nchini Marekani, baada ya taarifa kusambaa zikidai kuonekana kwa mamba watatu wakizurura ndani ya eneo la mazoezi.

Kwa mujibu wa ripoti hizo, kambi hiyo iliyopo jimbo la Florida inadaiwa kuwa karibu moja kwa moja na ziwa, jambo ambalo linaaminika kuwa huenda liliwaruhusu wanyama hao kuingia katika eneo la uwanja wa mazoezi.

Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo lilisababisha wachezaji na benchi la ufundi kuchukua tahadhari kubwa, huku mazoezi yakidaiwa kusitishwa kwa muda mfupi ili kuhakikisha usalama wa wote waliopo kambini.

Ureno wako kundi ambapo mchezo wao wa kwanza watacheza dhidi ya DR Congo Juni 17 jiji la Houston


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.