Refa wa Kariakoo Derby aingia kwenye historia kombe la Dunia

Joel JJ By Joel JJ β€’ 9th June 2026


Refa wa Kariakoo Derby aingia kwenye historia kombe la Dunia

Aliyechezesha dabi ya Kariakoo Juni 25 2025 kati ya Yanga dhidi ya Simba msimu uliopita, mwamuzi wa kimataifa kutoka Misri, Amin Omar, ameingia kwenye historia ya waamuzi barani Afrika baada ya kuteuliwa kuchezesha miongoni mwa mechi za Kombe la Dunia 2026.

Omar atakuwa mwamuzi wa kati kwenye mechi kati ya Korea Kusini dhid ya Jamhuri ya Czech itakayochezwa Ijumaa, Juni 12.

Uteuzi huo unamfanya kuwa mmoja wa waamuzi wa Afrika waliopata nafasi kubwa zaidi kwenye michuano hiyo inayofanyika nchi za Mexico, Canada na Marekani.

Amin Omar huenda akawa miongoni mwa waamuzi watakaohusika katika mechi muhimu zaidi za Kombe la Dunia 2026.

Katika mechi hiyo, Amin Omar hatakuwa peke yake kutoka Misri. Mwamuzi mwenzake, Mahmoud Ashour, naye atakuwa sehemu ya kikosi cha waamuzi, akisimamia mfumo wa usaidizi wa video (VAR).


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.