Mgunda atua Simba

Joel JJ By Joel JJ β€’ 15th August 2026


Mgunda atua Simba

Simba SC imemtambulisha rasmi mshambuliaji Ismail Mgunda kuwa mchezaji mpya wa Wekundu wa Msimbazi, akitokea Mashujaa FC.

Mgunda anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Simba kuelekea msimu wa 2026/27.

Nyota huyo amejumuishwa kwenye kikosi cha Simba kilichosafiri Kagera tayari wa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa kesho Jumapili kwenye uwanja wa Kaitaba.

Anaungana na Ibrahim Doumbia kuongoza jahazi la Simba eneo la washambuliaji wa kati


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.