Azam Fc kuanzia ugenini Arusha dhidi ya Fountain Gate baada ya FIFA break

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th June 2026


Azam Fc kuanzia ugenini Arusha dhidi ya Fountain Gate baada ya FIFA break

Klabu ya Azam FC imeondoka mapema leo kuelekea mkoani Arusha, ikiwa tayari kwa mchezo wake wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Fountain Gate FC utakaopigwa baada ya mapumziko ya kimataifa ya FIFA.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa tarehe 12 Juni 2026 katika Uwanja wa Shikh Amri Abeid Kaluta, kuanzia saa 10:00 jioni, huku ukitarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na umuhimu wake kwa msimamo wa ligi.

Azam FC inaingia kwenye mchezo huo ikiwa katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi, ikiwa imekusanya pointi 52 hadi sasa. Timu hiyo inaendelea kupambana kusalia kwenye mbio za ubingwa au nafasi za juu, huku kila mchezo ukiwa na uzito mkubwa katika hatua hii ya msimu.

Kwa upande mwingine, Fountain Gate FC inashika nafasi ya tisa kwenye msimamo ikiwa na pointi 29. Timu hiyo itakuwa nyumbani Arusha ikitafuta matokeo mazuri ili kuboresha nafasi yake na kuepuka presha ya chini ya msimamo.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.