Yona Amos kutua Singida Black Stars

Joel JJ By Joel JJ β€’ 10th June 2026


Yona Amos kutua Singida Black Stars

Mlinda lango Yonah Amos anatarajiwa kujiunga na Singida Black Stars akitokea Pamba Jiji baada ya kukamilisha makubaliano ya kimkataba na walima alizeti hao.

Taarifa zilizopatikana zinaeleza kuwa pande zote mbili zimekamilisha taratibu za mwisho za usajili, huku nyaraka za mkataba zikiwa zimeshasainiwa rasmi, hatua inayomfanya kipa huyo kuwa mchezaji mpya wa Singida Black Stars kuanzia msimu ujao.

Yonah anaondoka Pamba Jiji mwishoni mwa msimu huu baada ya mkataba wake kumalizika, hivyo kuhitimisha kipindi chake ndani ya klabu hiyo ya Mwanza aliyoitumikia kwa misimu miwili.

Uamuzi wa Singida Black Stars kumsajili Yonah unaonekana kuwa sehemu ya mkakati wa kuimarisha kikosi chao kuelekea msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC pamoja na mashindano mengine watakayoshiriki.

Klabu hiyo imeendelea kujijenga kama moja ya timu zinazovutia wachezaji wenye uwezo mkubwa nchini Tanzania katika kipindi cha hivi karibuni. Singida Black Stars pia imekuwa miongoni mwa timu zilizokuwa na ushindani mkubwa katika Ligi Kuu Tanzania Bara na imeendelea kuwekeza kwenye kikosi chake.


  

XTRA 90 INSIDER

Get the latest tactics & rumors delivered to your inbox.